Mourinho adai hela aliyotumia kukijenga kikosi chake ni ndogo!

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amedai kuwa dau la £300m alilotumia kuimarisha kikosi chake halitoshi baada ya timu yake kutoka sare ya 2-2 na klabu ya Burnley siku ya Jumanne.
Jesse Lingard alifunga katika dakika za lala salama kusawazisha, na sasa sare hiyo inaiwacha Man United ikiwa pointi 12 nyuma ya viongozi wa ligi ManCity. ”Tuko katika mwaka wa pili kujaribu kujenga timu ambayo unajua sio miongoni mwa timu bora duniani”, alisema raia huyo wa Ureno. ”Manchester City inanunua mabeki wa kushoto na kulia kwa gharama ya washambuliaji, aliongezea”. Mourinho ambaye aliteuliwa kuwa mufunzi wa United mnamo mwezi Mei 2016 na kuvunja rekodi ya dunia alipomnunua kiungo wa kati Paul Pogba kwa kitita cha £89m, Eric Bailly kwa kitita cha £30m na kiungo wa kati Henrikh Mkhitaryan kwa £26.3m. Mourinho aliulizwa iwapo alama nane katika mechi tano zinatosha kwa klabu kama Man United. Alijibu: Unaposema klabu kama United , je nadhani Milan sio klabu kubwa kama sisi?Unadhani Real Madrid sio klabu kubwa kama yetu?.

No comments

Powered by Blogger.